Walipokuwa Bethlehemu, wakati wa Mariamu kujifungua uli fika, naye akamzaa mtoto wa kiume, kifungua mimba. Akamfunika kwa vinguo na kumlaza horini, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.
Usiku ule walikuwako wachungaji wakilinda kondoo zao nje ya mji. Ghafla malaika wa Bwana akawatokea, na utukufu wa Mungu ukawang'azia pande zote. Wakajawa na hofu kuu. Lakini malaika akawatuliza akisema: ``Msiogope! Nawaletea habari njema ya furaha kubwa, na habari hii ni kwa faida ya watu wote! Kwa maana leo katika mji wa Bethlehemu, amezaliwa Mwokozi ambaye ndiye Kristo Bwana. Na hivi ndivyo mtakavyomtambua: mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa vinguo na kulazwa horini.''Mara jeshi kubwa la malaika wa mbinguni likatokea na pamoja wakamsifu Mungu wakiimba:``Atukuzwe Mungu juu mbin guni, na duniani iwepo amani kwa watu ambao amependezwa nao.''
Malaika hao waliporudi mbinguni wale wachungaji walish auriana: ``Jamani, twendeni Bethlehemu tukaone mambo haya ya ajabu yaliyotokea, ambayo Bwana ametufahamisha.''
Kwa hiyo wakaenda haraka Bethlehemu, wakawakuta Mariamu na Yusufu; na yule mtoto mchanga alikuwa amelala mahali pa kulia ng'ombe. Walipomwona mtoto, wakawaeleza yale waliyokuwa wameambiwa. Na wote waliosikia habari hizi wakastaajabia yale waliyoambiwa na wachungaji.Lakini Mariamu akayaweka mambo haya yote moyoni mwake, akayafikiria mara kwa mara.
Wale wachungaji wakarudi, huku wakimtukuza Mungu na kum sifu kwa yale waliyoyasikia na kuyaona.
Merry Christmas!
Jonathan for the Ferguson Family